Namna ya kuishi kwa amani kwenye ndoa


 Kuna msemo unasema raha jipe mwenyewe nimeuelewa kwenye mtazamo huu ,Katika maisha haya ya mpito lazima kuhakikisha kuwa unaamani na furaha na ,hakika furaha ya mtu huondolewa na mtu.Kwa mantiki hiyo yatupasa kuhakikisha kuwa mtu anapotuingilia katika amani na furaha yatupasa kuhisi kuwa mtu huyo anasumbuliwa na kitu fulani na kumsamehe na kupuuza inapowezekana ili kuilinda amani yetu na furaha.

     Kumbuka pia kuwa ukiwa hauna amani na furaha basi utasababisha mwili hisia na akili kwenda isivyo na kuwa na mrundikamo wa mambo yasiyo na suluhu na kusababisha mwili kujihami na kuharibu mfumo wote wa mwili ,mwisho wake utajikuta hospitali au unaweza kukonda,kuharisha na kutapika pasipo sababu .Kwa nini mtu anakuwa na madonda ya tumbo ,au kichaa.Mara nyingi watu hupatwa na madonda tumbo kwa ajili ya mawazo na kusababisha kifo .Watu wengi hufa sababu ya Kukosa furaha na amani yaani huwaza mambo wasiyokuwa na majibu yake.Unapofikia hatua ambayo ni mwisho na huwezi kuendelea basi hapo mwambie aliekuumba akusaidie na afungue njia ili upite.

Jitahidi kuwa na furaha wakati wote 

Comments

Popular Posts