NDOA NA UKWE NI SHIDA

Madhara ya kukaa nyumbani kwa wazazi ungali umekwisha kuowa ni makubwa sana.Mara zote huwa ninashauri kuwa kila mtu na awe na kwake hizi habari za kukaa sehemu moja ni mfumo wa mifugo lakini binadamu yeyote anapaswa kuwa na kwake .Kwa nini niseme kuwa kila mtu na awe na kwake ?Sababu ziko nyingi lakini niseme chache.Moja ya sababu ni kuwa kila mwanadamu anao utashi wake,malengo na mtazamo wake binafsi na binadamu huwa anazo ndoto kuwa anataka kuwaje katika maisha .Umoja mwingi hufa na kuingia migogoro mara baada ya kutokuwa na mtazamo mmoja.Mamlaka kila mmoja anayo mamlaka ya kupanga kipi kiende hivi na kingine kiende vile sasa kama uko kwenu umefugwa ukitaka kitu kiende hivi mwenye mamlaka yaani mfugaji wako atakataa na kukuhisi kuwa unampinga,na hapo migogoro ndipo huanzia .Wazazi wanaofuga watoto wao huwa wanawasingizia sana wakwe zao kuwa wao ndiyo kikwazo maana baada ya kuowa tu mwanaume huanza kuona madhala ya kufugwa kwao maana faida nyingi itakuwa ya wanaomfuga yaani wazazi.Moyo wake huanza kutafuta uhuru na kwa sababu anatazamwa kama kikwazo ni mkamwana basi ataandamwa sana na mwanaume asipokuwa na msimamo aweza kumwacha mke kwa masilahi ya wafugaji wake .

Mwanaume akiowa mke lazima atahitaji kumtunza mkewe atamnunulia vitu na kumlinda kama mwenzake.Familia yake yani wazazi mara nyingi huwa hawapendi na kuanzisha fujo. Itaendelea



Comments

Popular Posts