NDOA NI UWANJA WA VITA
NDOA NI UWANJA WA VITA
SEHEMU YA KWANZA
Na Jackson M Kuhenda
Ndoa ilianza zamani sana huko eden, alieianzisha alikuwa ni Mfalme wa ajabu, ninasema wa ajabu maana Yeye pekee ndiye awezaye kuumba hata leo. Alipendezwa kuumba kiumbe chenye muonekano kama ulivyo wewe, alikusudia wewe uishi kwa furaha katika maisha yako,na alipendezwa wewe ukiwa na mume au mke,na kuzaa wengine watakaooana kama wewe na kufurahia milele.Kusudi la kuishi wawili ilikuwa ni kufarijiana,na kuelekezana pia kusaidiana.Kama ni hivyo kwa nini imekuwa uwanja wa vita?. Jibu ni kuwa alikuwepo kiumbe mmoja jina lake anaitwa Lusifer Alikuwa ni mtumishi wa huyo Mfalme muumbaji ambaye naye aliumbwa kama sisi, alitamani nae kuwa mfalme, japo Mfalme alikuwa mmoja tu,naye ni muumbaji wetu. Huyo Lusifer alianza njama za kupindua ufalme, alionywa mara kadhaa lakini Lusifer hakughaili mwisho ikatokea vita na Lusifer akapigwa na kushikwa kisha kufukuzwa ikulu akawa anatanga tanga huku na kule mwisho akaingia katika ndoa, akawakosanisha wanandoa na Mfalme wao akitaka wafe na atawale sehemu waliyokuwa wanaishi wanandoa hao.Lusifer alifanikiwa kwa kuwalaghai wanandoa,na walifaa kufa lakini Mfalme akafanya mpango wa kulipa fidia ili wanandoa waishi tena na baada ya kulipa deni Mfalme aliwataka wanandoa na familia kwa ujumla wadhihilishe kama wanataka kuishi milele na akawaelekeza kanuni za kujipima kama wanafaa. Sasa hapo kwenye kudhihilisha ndo Lusifer anapigana kuwaangusha wanafamilia ili wasifae kuishi milele wakati utakapofika, anapigana kuhakikisha ndoa na familia kunakuwepo migogoro, na anataka ndoa ionekane kama ni mpango mbaya na watu wafanye uasherati na uzinzi, na wafanye matendo ya kuihalamisha ndoa waoane jinsia moja, waowe ama kuowa wanyama nk. Kwa ufupi ndoa haina mvuto na maana sababu ya ushindani wa Lusifer na Mfalme Lusifer ndiye Ibilisi na Shetani, na Mfalme ndiye Mungu muumbaji wetu. Usikatae ndoa na utaukubali mpango wa Mungu na jua yupo adui aliefanikiwa sana kudanganya na utamshinda kwa kuijua kweli na kuisimamia. Hapo utakuwa na ushindi katika ndoa yako na mpango ukikamilika uishi milele. Ufafanuzi Ikulu ni mbinguni


Comments
Post a Comment