FAIDA NA HASARA YA MAHUSIANO

Ona


  • Faida na hasara ya mahusiano. 
  • Na Jackson Michael
  • Tunapozungumzia mahusiano tunamaanisha ni Ile hali ya kuwa karibu, kwa wachumba, wanandoa pia jamii. Kuhusiana ni kushirikiana kutiana moyo, kifarijiana,kuelekezana,kufundishana,kuonyana, kukubaliana, kupongezana,. Kwa ufupi ni kutenda mambo kwa umoja, hiyo ndiyo mahusiano.Na hii kwa wachumba huleta matokeo ya ndoa, kupeana mimba au kutoroshana.Vijana mjitahidi kukaa mbali na wachumba wasichana ogopa kukaa karibu na wavulana hasa maeneo ya faragha kuepuka kubakwa au kushawishiwa kutenda ngono kabla ya ndoa
  • Ndoa ni jambo jema na huleta furaha na uhusiano mwema kwa 
  • (1)wazazi
  • (2)ndugu 
  • (3) jamii kwa ujumla.
  • Mimba ni jambo jema na la heshima kwa wanandoa mwanamke anapobeba ujauzito na hatimae kupata mtoto. Kwanza wanandoa hupewa heshima na kuonekana kama ni wanajamii bora, na mtoto pia hupata heshima sawasawa na wazazi. Lakini mimba ikipatikana nje ya ndoa huwafanya wazazi hao watalajiwa kuonekana kuwa ni watu wasiofaa kuheshimika na hudharauliwa sana na kutengwa kama watu waharibifu na wavunjaji wa maadili. Nawasihi vijana na watu wazima mjitahidi kuepuka hii hali maana inaleta utata katika jamii yetu. 
  • Kutoroshana nalo siyo jambo jema maana ni kuvunja taratibu,na kawaida ya binadamu jinsi tulivyo kuoa au kuolewa huleta mahusiano ya kifamilia kati ya familia ya mwanaume na ya mwanamke. Kutoroshana huchochea uhasama kati familia hizo na kuwa maadui labda mpaka muowaji aombe samahani kupitia wazazi au ndugu kisha kutoa faini na kutoa mahali au kutotoa sawasawa na makubaliano. Tujitahidi kuwa na mahusiano bora katika ndoa kisha kwa ndugu na kwa jamii pia asante

Comments

Popular Posts