DAWA YA KUACHA KUCHEPUKA
Kuchepuka siyo suluhisho la changamoto zako za ndoa na maisha ya pamoja.Watu wengi wamekuwa wakiponzwa na kusimama mguu mmoja nje na mwingine ndani.Kwa sababu utakuta mtu yuko na mke au mume lakini akajikuta anatamani mke au mume wa kando au jilani.Wengi hutoa visingizio kuwa,wao hawachepuki lakini mwenzie yeye huchepuka.Na wakati mwingine huwa nawauliza maswali kuwa je ulimuona umeambiwa au unahisi?.Wengi huwa ni watu wa kuhisi tu na wengine husema kuwa waliona na kumbe hakuona.Kwa nini husingizia ,sababu ni kuwa watu wengi kulala na wanaume au wanawake aina mbalimbali ni tabia yao na hutafuta vichaka ili waonekane kama vile wanayo haki ya kuchepuka kumbe ni tamaa tu.Sasa nataka niseme na wanandoa kuwa inawezekana kutochepuka na hakuna madhala yoyote ya kutochepuka ,hivyo kila mtu aweza kuishi bila kuchepuka akitaka.Madhala ya kuchepuka ni mengi na husababisha vifo,visasi,lawama ,ugomvi,na umasikini na huondoa mibaraka ya ndoa na heshima huwa haipo kwa mji wa mchepukaji.Maendeleo huwa dhaifu kwa mchepukaji hata kama yatakuwepo basi ujue yangekuwa zaidi kama kusingekuwa na hiyo tabia ya kishetani.Wito kama wewe unataka ubarikiwe na Mungu,na ndoa yako iwe na mafanikio basi acha hii tabia nawe utakuwa huru na hutakuwa na wasiwasi tena katika ndoa yako na utaona thamani ya mwenzio na utaona raha kuwa nae maana wanasema mtu anayo nafasi moja ya upendo katika mahusiano,akiwa nao wawili lazima atampenda mmoja na kumtelekeza mmoja na hapo ndipo tatizo lilipo



Comments
Post a Comment