MWANAMKE MZURI LAZIMA AOLEWE
Mwanamke mzuri kuolewa ni lazima sababu ,mwanaume yeyote yule mwenye akili timamu lazima atataka aowe mwanamke mzuri.
Watu wengi huzani kuwa uzuri ni kuwa na ,sura nzuri,umbo zuri,maneno mazuri nk.Mie nachojua ni kuwa mwanamke mzuri ni yule mwenye dhamira safi,nia safi ,na moyo safi,mvumilivu na mwenye msimamo thabiti.Akiwa katika hali hii lazima atakuwa na tabia njema ,hapa ndipo tunapata kile kisemwacho kuwa mwanamke ni tabia .Ikiwa wewe unatabia mbaya maanayake lazima utaachika maana huna kiasi,msimamo ,na uvumilivu.Kwa hali isiyo nzuri lazima ndoa ikushinde.Uvumilivu na mengine daima huletwa na malengo.Ikiwa ni lengo lako kuolewa lazima usimamie malengo yako na hiyo itakupa nguvu kutatua changamoto njiani.
Kumbuka kuwa mtu alieolewa anayo heshima kubwa kwenye jamii kuliko asieolewa jiunge na jamii inayoaminika na kuheshimika ukae na mumeo muda wote



Comments
Post a Comment