WASIWASI NI ADUI MKUBWA WA MAHUSIANO
Wasiwasi kwenye mahusiano ni jambo baya ,ukitaka kuishi kwa amani kwenye ndoa basi yapaswa mwenzi wako akuamini,Ukiaminika utakuwa na furaha na utalindwa.Mwenzi wako asipokuamini basi ataishi nawe akiwa na wasiwasi na kamwe hataweka tumaini lolote kwako.Atakachokifanya ni kujiandaa KUACHA au kuachwa.
Wasiwasi huletwa na mienendo isiyo mizuri au muonekano wenye viashilia vya tabia mbaya.Mfano uzinzi,uongo,utapeli wizi nk.Binadamu ni rahisi sana kumgundua akiwa ni mzinzi utaona tu nyenendo zisizo za kawaida na utakuwa ukiona tabia ngeni machoni pako.Uzinzi pia huzalisha uongo.Utaona unaambiwa habari za kiongo kabisa na ukichunguza hautachelewa kuona siri iliyonyuma ya pazia .Utadanganywa hata kuwepo kwa misiba safari za kushtukiza na mengine mengi.Na hayo yote huleta wasi wasi mara "nimejikwaa nimechubuka" kumbe kafumaniwa au alichubuka wakati wa uzinzi wake.Mara "nguo yangu ilishikwa na mti ikachanika".
Mwanaume na mwanamke toshekeni na mmoja na akili yako ihame kwenye ngono ,bali ielekee kwenye maendeleo ya familia.Kwa kufanya hayo utapata amani na utakuwa na furaha tele moyoni mwako.



Comments
Post a Comment