UTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILEILE

Uzuri wa mwanamke ni tabia, na uzuri wa sura na umbo ni macho yako tu.Unaweza kusumbuliwa na mapambo na makava ya kubumba lakini mwanamke ni mwanamke.
Mwanaume mmoja aliyekuwa anajuta mara baada ya kusumbuliwa na mke mpya aliemuowa kwa ghalama kumbwa na kuandaa harusi kubwa .Alimuacha mke wake aliekuwa amezaa nae na kuishi nae kwa muda mrefu ,walikuwa wamezoeana na walivumiliana .Aliamua kuowa mke mpya mara baada ya kuchekwa na rafiki zake wakisema,''Wewe na ujanja wote huo unaishi na mwanamke yule''Aliamua kuowa mwanamke mzuri wa sura akamuacha mzuri wa tabia .Sasa ameamua kumrudia mke wake wa zamani liwalo na liwe maana hakuna kipya isipokuwa sura tu .Nimemsifu sana ungekuwa wewe ungemshaurije?.

Comments

Popular Posts