KUBALI KOSA NA UJIREKEBISHE


 Kuna wakati mateso tunayakubali yatutese na kutufanya tuhisi kutengwa sababu tu sisi wenyewe hatutaki kukubali na kuacha njia zetu mbaya . Kamwe usitegemee kupata amani ya kweli kutoka kwenye mahusiano ya kindoa,Familia au jamii ,kama utakuwa mtu anaeendea njia mbaya.Mfano ukawepo kwenye ndoa harafu ukawa malaya,hapo tegemea mshahara wa ulichokipanda haiwezekani mwenzio akugundue kuwa wewe ni malaya harafu anyamaze na kuridhika.Kama atanyamaza na kuridhika basi ujue kuna sababu iliyosababisha anyamaze,nayo yaweza kuwa anakuchunguza apate ukweli au anakupa muda ujirekebishe yaani uacha kabla hajakufuma nk.Kinyume chake jua kuwa ndoa yako haitadumu na kuwa na amani.Kijamii pia kama wewe ni mharifu lazima jamii ikupe kundi lako na watakuandama kwa shutuma za kile unachokifanya .Suruhu ni kuacha njia mbaya na hapo ndipo mambo yako yataenda vyema na Mungu atakuwa msaada wa karibu kwako.

Comments

Popular Posts