FAMILIA KUBWA NI CHANZO CHA MIGOGORO
Na Jackson Michael Kuhenda
Moja ya sababu za migogoro katika familia huletwa na watu wanaohifadhiwa kwenye kapu linaloitwa familia.Ni ukweli usiopingika kuwa familia ni mali ya mume na mke na hapa huibuka tatizo jingine kubwa kuwa,baadhi ya mila na tamaduni zetu zinalazimisha kuwa mwanamke awe ni mtu asiye na mamlaka katika familia,Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa imekuwa ni ngumu sana familia kuendesheka ikiwa baba atalazimisha kuwa mtawala,anaetumia mabavu yaani anatawala kwa nguvu na siyo demokrasia Baadhi ya wanaume wamekuwa wakiuawa kwa sababu ya kutangaza utawala au umiliki wa upande mmoja.Imeonekana hata mali wanaume baadhi wamekuwa wakitangaza kuwa ni zao binafsi na kuonyesha kuwa wanawake ni kama watumwa waliokuja kutumika na siyo kujenga familia na kuchochea maendeleo ya pamoja.Hali hii ya ubinafsi ndiyo imeleta mpambano na harakati za kila mmoja apate chake.
Nafikili kuwa mambo haya yanachanzo chake na inapaswa kurudi kwenye chanzo na kusahihisha na kuanza upya.Ni kweli kuwa Mungu alisema mwanamke atatawaliwa lakini hakumnyima kumiliki familia na mali sema atazimiliki kupitia mume wake nae atasimamiwa kuzitumia vyema kwa masilahi mapana ya familia.Mke mwema amesemwa kuwa ni kama merikebu inayoleta mali kutoka mbali na nimzuiaji wa wafujaji, wahujumu uchumi wa familia na nimlinzi wa vyote vilivyopo katika familia.Kwa kufanya hivyo amekuwa akipata tuhuma nyingi kutoka kwa wahujumu uchumi ambao waweza kuwa wazazi,mawifi makaka au ndugu na jamaa waliopo nyumbani au wanaolizunguka familia kimasilahi.Kama unataka kuishi vyema na mke na ndugu zako usiwe mwepesi wa kuamua ukisikia jambo chunguza ujue undani wake hata kama limetendeka mbele yako. Inawezekana kukawa na hila ndani yake na aliyetenda hayo ni mtu nae kazidiwa na mtihani unaweza ukakuta kumbe ndiyo alikuwa upande wako ila watu wakamcholea mchora ili aumbuke na aondoke kisha lengo lao lifanikiwe.Mungu akupe nguvu unapoishi kwenye familia kubwa.



Comments
Post a Comment