HEKIMA NI DAWA KWENYE MAHUSIANO

Hekima ni uwezo ama akili ya kuweza kutambua lipi jema na ovu ,kujua lipi ni ukweli na kipi ni uongo.Wacha Mungu pote duniani huamini kuwa ,Hekima ni zawadi ambayo mtu aweza kupewa akiwa upande wa Mungu .Hii iko tofauti kidogo na Akili ya darasani au kupewa na anaejua jambo unalopewa .

Hekima au uwezo wa kung'amua mambo huweza kumfanya atambue kuwa kilichotendeka Kiko sawa na maelezo au kuna kitu kimefichwa na kama kimefichwa ajue nini cha kufanya.Na cha kufanya ni kuhakikisha mambo hayaharibiki na kuleta madhala makubwa.

Mwanamke na mwanaume mwenye Hekima huwa na mafanikio mazuri na hujiepusha na maovu mengi wakiondoa tu utashi wao.
 
Ni vyema kuowa au kuolewa na mtu mwenye hekima.Mtu mwenye hekima utamgundua kwa kuwa mchaji wa kweli wa Mungu.Nachomaanisha hapa ni mtu anaeujua ukweli kuhusu Mungu na anautumainia.


Ukiwa unaishi na mtu mwenye hekima yakupasa uwe mkweli na msamaha utumike kweli na usiwe na hila katika kuomba msamaha,yaani usiombe msamaha ili kumridhisha tu.

Comments

Popular Posts